Comments

Ambaye Wolde Michael Dr.

Share this
25.March

Dk. Ambaye Wolde Michael ni daktari mwenye uzoefu wa kufanya operesheni ya fistula aliyesomea Sayansi ya Tiba ya Uzazi na Magonjwa ya Wanawake kwenye Chuo Kikuu cha Addis Ababa nchini Ethiopia, kisha akafanya kazi kama daktari wa fistula kwenye Hospitali ya Addis Ababa kwa miaka 14. Katika kipindi hicho amewafanyia operesheni wanawake zaidi ya elfu tano na kupata uzoefu wa kushughulikia matatizo makubwa ya fistula ya uzazi na kuyatibu. Anayo pia shahada ya umahiri katika afya ya jamii kutoka Chuo Kikuu cha Leeds cha nchini Uingereza.

Dk. Ambaye amezitembelea nchi kadhaa zinazoendelea barani Afrika na Asia na kutoa mafunzo ya operesheni ya fistula kwa madaktari wengi. Ameshiriki kwenye mikutano na warsha nyingi za kimataifa akitoa mada na uzoefu wake kwenye fani hii ambako ni mahiri. Kabla ya kujiunga na kikosi cha WAHA nchini Ethiopia, alikuwa akifanya kazi binafsi ya kutoa ushauri wa kitaalamu na kuendesha programu za mafunzo kwenye masuala ya afya ya uzazi kwa wanawake ikiwemo fistula ya uzazi, huduma za dharura za uzazi, na kadhalika. Hivi karibuni zaidi, Dk. Ambaye alikuwa akifanya kazi kama mshauri wa kimataifa wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloratibu masuala ya idadi ya watu, UNFPA, nchini Afghanistan akishughulikia masuala ya mafunzo kwa madaktari wazalishaji na wa magonjwa ya wanawake katika kutibu fistula na kuendeleza mtaala wa programu ya mafunzo ya fistula ya uzazi.


Sitemap